Uchaguzi wa Mistari ya Biblia inayo husu upendo
Uchaguzi wa Mistari ya Biblia inayo husu upendo
Uchaguzi huu ni mwongozo, wenye mistari yote ya msingi
juu ya somo UPENDO. Huu siyo mbadala wa kusoma Biblia yote, bali
inatusaidia kukumbuka na kupata uhakika juu ya imani yetu. Ni matumaini
yangu kuwa utatiwa moyo na utaimarishwa.
- Basi, sasa inadumu imani, tumaini, upendo, haya matatu; na katika hayo lililo kuu ni upendo. -
[1 Wakorintho 13:13]
-
Akamwambia, Mpende Bwana Mungu wako kwa moyo wako wote, na kwa roho yako
yote, na kwa akili zako zote. Hii ndiyo amri iliyo kuu, tena ni ya
kwanza. Na ya pili yafanana nayo, nayo ni hii, Mpende jirani yako kama
nafsi yako. Katika amri hizi mbili hutegemea torati yote na manabii. -
[Mathayo 22:37-40]
-
Kwa maana jinsi hii Mungu aliupenda ulimwengu, hata akamtoa Mwanawe
pekee, ili kila mtu amwaminiye asipotee, bali awe na uzima wa milele. -
[Yohana 3:16]
-
Zaidi ya yote iweni na juhudi nyingi katika kupendana; kwa sababu upendano husitiri wingi wa dhambi. -
[1 Petro 4:8]
-
Katika hili tumelifahamu pendo, kwa kuwa yeye aliutoa uhai wake kwa
ajili yetu; imetupasa na sisi kuutoa uhai wetu kwa ajili ya hao ndugu.
Lakini mtu akiwa na riziki ya dunia, kisha akamwona ndugu yake ni
mhitaji, akamzuilia huruma zake, je! Upendo wa Mungu wakaaje ndani yake
huyo? Watoto wadogo, tusipende kwa neno, wala kwa ulimi, bali kwa tendo
na kweli. -
[1 Yohana 3:16-18]
-
Wapenzi, na mpendane; kwa kuwa pendo latoka kwa Mungu, na kila apendaye
amezaliwa na Mungu, naye anamjua Mungu. Yeye asiyependa, hakumjua Mungu,
kwa maana Mungu ni upendo. -
[1 Yohana 4:7,8]
-
Maana torati yote imetimilika katika neno moja, nalo ni hili, Umpende jirani yako kama nafsi yako. -
[Wagalatia 5:14]
-
Mkinipenda, mtazishika amri zangu. -
[Yohana 14:15]
-
Na Mfalme atajibu, akiwaambia, Amin, nawaambia, kadiri mlivyomtendea
mmojawapo wa hao ndugu zangu walio wadogo, mlinitendea mimi. -
[Mathayo 25:40b]
-
Basi yo yote myatakayo mtendewe na watu, nanyi watendeeni vivyo hivyo; maana hiyo ndiyo torati na manabii. -
[Mathayo 7:12]
-
Mkichukuliana, na kusameheana, mtu akiwa na sababu ya kumlaumu mwenzake;
kama Bwana alivyowasamehe ninyi, vivyo na ninyi. Zaidi ya hayo yote
jivikeni upendo, ndio kifungo cha ukamilifu. -
[Wakolosai 3:13,14]
-
Mambo yenu yote na yatendeke katika upendo. -
[1 Wakorintho 16:14]
-
Hakuna aliye na upendo mwingi kuliko huu, wa mtu kuutoa uhai wake kwa ajili ya rafiki zake. -
[Yohana 15:13]
-
Sisi twapenda kwa maana yeye alitupenda sisi kwanza. -
[1 Yohana 4:19]
-
Kwa maana nimekwisha kujua hakika ya kwamba, wala mauti, wala uzima,
wala malaika, wala wenye mamlaka, wala yaliyopo, wala yatakayokuwapo,
wala wenye uwezo, wala yaliyo juu, wala yaliyo chini, wala kiumbe
kinginecho chote hakitaweza kututenga na upendo wa Mungu ulio katika
Kristo Yesu Bwana wetu. -
[Warumi 8:38,39]
-
Amri mpya nawapa, Mpendane. Kama vile nilivyowapenda ninyi, nanyi mpendane vivyo hivyo. -
[Yohana 13:34]
-
Yeye aliye na amri zangu, na kuzishika, yeye ndiye anipendaye; naye
anipendaye atapendwa na Baba yangu; nami nitampenda na kujidhihirisha
kwake. Yuda (siye Iskariote), akamwambia, Bwana, imekuwaje ya kwamba
wataka kujidhihirisha kwetu, wala si kwa ulimwengu? Yesu akajibu,
akamwambia, Mtu akinipenda, atalishika neno langu; na Baba yangu
atampenda; nasi tutakuja kwake, na kufanya makao kwake. Mtu
asiyenipenda, yeye hayashiki maneno yangu; nalo neno mnalolisikia silo
langu, ila ni lake Baba aliyenipeleka. -
[Yohana 14:21-24]
-
Pendo na lisiwe na unafiki lichukieni lililo ovu, mkiambatana na lililo jema. -
[Warumi 12:9]
-
Wapenzi ikiwa Mungu alitupenda sisi hivi, imetupasa na sisi kupendana. -
[1 Yohana 4:11]
-
Na amri hii tumepewa na yeye, ya kwamba yeye ampendaye Mungu, ampende na ndugu yake. -
[1 Yohana 4:21]
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni