Uchaguzi wa Mistari ya Biblia kuhusu somo msamaha
Uchaguzi wa Mistari ya Biblia kuhusu somo msamaha
Uchaguzi
huu ni mwongozo, wenye mistari yote ya msingi juu ya somo la msamaha
.watu wengi wameshindwa kusamehe na kusahau sababu ya kukuso msingi
mzuri wa neno la mungu. Mungu akusaidie kupitia mistari hii uwasamehe
Adui zako kabisa na kusahau
- Kwa maana mkiwasamehe watu makosa yao, na Baba yenu wa mbinguni
atawasamehe ninyi. Bali msipowasamehe watu makosa yao, wala Baba yenu
hatawasamehe ninyi makosa yenu. -
[Mathayo 6:14,15]
-
Yesu akasema, Baba, uwasamehe, kwa kuwa hawajui watendalo. Wakagawa mavazi yake, wakipiga kura. -
[Luka 23:34a]
-
Akamwambia, Hakuna, Bwana. Yesu akamwambia, Wala mimi sikuhukumu. Enenda zako; wala usitende dhambi tena.]
- -
[Yohana 8:11b]
-
Mimi, naam, mimi, ndimi niyafutaye makosa yako kwa ajili yangu mwenyewe, wala sitazikumbuka dhambi zako. -
[Isaya 43:25]
-
Heri wenye rehema; Maana hao watapata rehema. -
[Mathayo 5:7]
-
Kwa sababu nitawasamehe maovu yao, Na dhambi zao sitazikumbuka tena. -
[Waebrania 8:12]
-
Kisha Petro akamwendea akamwambia, Bwana, ndugu yangu anikose mara ngapi
nami nimsamehe? Hata mara saba? Yesu akamwambia, Sikuambii hata mara
saba, bali hata saba mara sabini. -
[Mathayo 18:21,22]
-
Tukiziungama dhambi zetu, Yeye ni mwaminifu na wa haki hata atuondolee dhambi zetu, na kutusafisha na udhalimu wote. -
[1 Yohana 1:9]
-
Kama mashariki ilivyo mbali na magharibi, Ndivyo alivyoweka dhambi zetu mbali nasi. -
[Zaburi 103:12]
-
Usifanye kisasi, wala kuwa na kinyongo juu ya wana wa watu wako; bali umpende jirani yako kama nafsi yako; Mimi ndimi Bwana. -
[Mambo ya Walawi 19:18]
-
Kwa mtu mwenye fadhili utakuwa mwenye fadhili; Kwa mkamilifu utajionyesha kuwa mkamilifu; -
[Zaburi 18:25]
-
Kwa maana Wewe, Bwana, U mwema, Umekuwa tayari kusamehe, Na mwingi wa fadhili, Kwa watu wote wakuitao. -
[Zaburi 86:5]
-
Rehema na kweli zisifarakane nawe; Zifunge shingoni mwako; Ziandike juu
ya kibao cha moyo wako. Ndivyo utakavyopata kibali na akili nzuri, Mbele
za Mungu na mbele ya mwanadamu. -
[Mithali 3:3,4]
-
Ndivyo na Baba yangu wa mbinguni atakavyowatenda ninyi, msiposamehe kwa mioyo yenu kila mtu ndugu yake. -
[Mathayo 18:35]
-
Nanyi, kila msimamapo na kusali, sameheni, mkiwa na neno juu ya mtu; ili
na Baba yenu aliye mbinguni awasamehe na ninyi makosa yenu. -
[Marko 11:25]
-
Msihukumu, nanyi hamtahukumiwa; msilaumu, nanyi hamtalaumiwa; achilieni, nanyi mtaachiliwa. -
[Luka 6:37]
-
tena iweni wafadhili ninyi kwa ninyi, wenye huruma, mkasameheane kama na Mungu katika Kristo alivyowasamehe ninyi. -
[Waefeso 4:32]
-
mkichukuliana, na kusameheana, mtu akiwa na sababu ya kumlaumu mwenzake; kama Bwana alivyowasamehe ninyi, vivyo na ninyi. -
[Wakolosai 3:13]
-
mkiangalia sana mtu asiipungukie neema ya Mungu; shina la uchungu lisije
likachipuka na kuwasumbua, na watu wengi wakatiwa unajisi kwa hilo. -
[Waebrania 12:15]
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni