Uchaguzi wa Mistari ya Biblia kuhusu somo la imani
Uchaguzi wa Mistari ya Biblia kuhusu somo la imani
Uchaguzi huu ni mwongozo, wenye mistari yote ya msingi juu ya somo la imani..kutokana na umuhimu wa imani katika mambo ya kiroho nimeamua kukuchambulia mistari michache tu kukusaidia kukua kwa imani yako katika Bwana .Mungu akusaidie upate kitu cha tofauti unaposoma mistari hii
- Basi imani, chanzo chake ni kusikia; na kusikia huja kwa neno la Kristo. -
[Warumi 10:17]
-
Mtumaini Bwana kwa moyo wako wote, Wala usizitegemee akili zako
mwenyewe; Katika njia zako zote mkiri yeye, Naye atayanyosha mapito
yako. -
[Mithali 3:5,6]
-
Yesu akamwambia, Ukiweza! Yote yawezekana kwake aaminiye. -
[Marko 9:23]
-
Hata imekuwa, mtu akiwa ndani ya Kristo amekuwa kiumbe kipya; ya kale yamepita tazama! Yamekuwa mapya. -
[2 Wakorintho 5:17]
-
kwa kuwa hakuna neno lisilowezekana kwa Mungu. -
[Luka 1:37]
-
Ndipo alipowagusa macho, akasema, Kwa kadiri ya imani yenu mpate. -
[Mathayo 9:29b]
-
Basi imani ni kuwa na hakika ya mambo yatarajiwayo, ni bayana ya mambo yasiyoonekana. -
[Waebrania 11:1]
-
Lakini mtu wa kwenu akipungukiwa na hekima, na aombe dua kwa Mungu,
awapaye wote, kwa ukarimu, wala hakemei; naye atapewa. Ila na aombe kwa
imani, pasipo shaka yo yote; maana mwenye shaka ni kama wimbi la bahari
lililochukuliwa na upepo, na kupeperushwa huku na huku. Maana mtu kama
yule asidhani ya kuwa atapokea kitu kwa Bwana. Mtu wa nia mbili
husita-sita katika njia zake zote. -
[Yakobo 1:5-8]
-
Lakini pasipo imani haiwezekani kumpendeza; kwa maana mtu amwendeaye
Mungu lazima aamini kwamba yeye yuko, na kwamba huwapa thawabu wale
wamtafutao. -
[Waebrania 11:6]
-
Maana kama vile mwili pasipo roho umekufa, vivyo hivyo na imani pasipo matendo imekufa. -
[Yakobo 2:26]
-
Na kila tendo lisilotoka katika imani ni dhambi. -
[Warumi 14:23b]
-
Lakini mwenye haki wangu ataishi kwa imani; Naye akisita-sita, roho yangu haina furaha naye. -
[Waebrania 10:38]
-
Tazama, ataniua; sina tumaini; ila hata hivyonitaithibitisha njia yangu mbele yake. -
[Ayubu 13:15a]
-
Nguvu zenu zitakuwa katika kutulia na kutumaini; lakini hamkukubali. -
[Isaya 30:15b]
-
Kama sisi hatuamini, yeye hudumu wa kuaminiwa. Kwa maana hawezi kujikana mwenyewe. -
[2 Timotheo 2:13]
-
Kwa maana kila kitu kilichozaliwa na Mungu huushinda ulimwengu; na huku ndiko kushinda kuushindako ulimwengu, hiyo imani yetu. -
[1 Yohana 5:4]
-
Zaidi ya yote mkiitwaa ngao ya imani, ambayo kwa hiyo mtaweza kuizima mishale yote yenye moto ya yule mwovu. -
[Waefeso 6:16]
-
Yesu akawaambia, Kwa sababu ya upungufu wa imani yenu. Kwa maana, amin,
nawaambia, Mkiwa na imani kiasi cha punje ya haradali mtauambia mlima
huu, Ondoka hapa uende kule; nao utaondoka; wala halitakuwako neno
lisilowezekana kwenu. -
[Mathayo 17:20]
-
tukimtazama Yesu, mwenye kuanzisha na mwenye kutimiza imani yetu; ambaye
kwa ajili ya furaha iliyowekwa mbele yake aliustahimili msalaba na
kuidharau aibu, naye ameketi mkono wa kuume wa kiti cha enzi cha Mungu. -
[Waebrania 12:2]
-
Basi tukiisha kuhesabiwa haki itokayo katika imani, na mwe na amani kwa Mungu, kwa njia ya Bwana wetu Yesu Kristo, -
[Warumi 5:1]
-
Yesu akajibu, akamwambia, Mwaminini Mungu. -
[Marko 11:22]
-
Mnafurahi sana wakati huo, ijapokuwa sasa kwa kitambo kidogo, ikiwa ni
lazima, mmehuzunishwa kwa majaribu ya namna mbalimbali; ili kwamba
kujaribiwa kwa imani yenu, ambayo ina thamani kuu kuliko dhahabu
ipoteayo, ijapokuwa hiyo hujaribiwa kwa moto, kuonekane kuwa kwenye sifa
na utukufu na heshima, katika kufunuliwa kwake Yesu Kristo. Naye
mwampenda, ijapokuwa hamkumwona; ambaye ijapokuwa hamwoni sasa,
mnamwamini; na kufurahi sana, kwa furaha isiyoneneka, yenye utukufu,
katika kuupokea mwisho wa imani yenu, yaani, wokovu wa roho zenu. -
[1 Petro 1:6-9]
Asante sana kwa somo zuri hakika nimepata kitu Mungu akubariki
JibuFuta